Mark 14:22-25

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:26-30; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

22 aWalipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”

23 bKisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.

24 cAkawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25 dAmin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”

Copyright information for SwhNEN